Genesis 27:30-35

30Baada ya Isaka kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni. 31Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”

32Isaka baba yake akamuuliza, “Wewe ni nani?”

Akajibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.”

33Isaka akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!”

34Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”

35Lakini akasema, “Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako.”

Copyright information for SwhKC